Michuano ya Ligi ya Mabingwa yarejea kwa kasi
2 Novemba 2020Katika kandanda la Ulaya, kutakuwa na mpambano wa miamba ambao wapo katika shinikizo. Real Madrid na Inter Milan huenda wana mataji 16 ya Ulaya kwa pamoja lakini wana shinikizo la mapema wakati watakapokutana katika mchuano wa tatu wa Champions League kesho.
hakuna timu iliyoonja ushindi mpaka sasa katika Kundi gumu la B ambalo pia lina Borussia Moenchengladbach na Shakhtar Donetsk ambao watakutana Ukraine.
Mabingwa watetezi Bayern Munich wanaendelea vizuri na watacheza dhidi ya RB Salzburg. Atletico Madrid itacheza dhidi ya Lokomotiv Moscow. Katika Kundi D, Liverpool itacheza dhidi ya Atalanta
Barcelona, ambao wanaongoza Kundi G watacheza Jumatano dhidi ya Dynamo Kiev. Juventus watakutana na washika mkia wa kundi hilo Ferencvaros.
Manchester United wanaongoza Kundi H na sasa watakutana na Basaksehir ya Uturuki. PSG itawaalika RB Leipzig katika marudio ya nusu fainali ya msimu uliopita ambapo walibwaga 3 bila.
Manchester City watacheza dhidi ya Olympiacos wakati mabingwa mara mbili Porto wakiwaalika Marseille.
Vinara wa Kundi F Lazio watacheza dhidi ya Zenit St Petersburg wakati Borussia Dortmund ikipambana na Club Brugge
Chelsea katika Kundi E itacheza dhidi ya Rennes na Sevilla itacheza dhidi ya Krasnodar.
Reuters, AFP, AP, DPA