1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miili 21 yafukuliwa katika eneo analomiliki mchungaji, Kenya

23 Aprili 2023

Polisi nchini Kenya imesema imefukua miili 21 hadi sasa katika eneo linalomilikiwa na mchungaji Paul Makenzi, aliyekamatwa na polisi baada ya kuwaagiza waumini wake kufunga hadi kufa.

https://p.dw.com/p/4QSUi
Kenia Kilifi | Exhumierung von Mitgliedern von Christlichem Kult durch Polizei
Picha: Stringer/REUTERS

Mkuu wa polisi katika kaunti ndogo ya Malindi, John Kemboi, amesema bado makaburi mengine katika eneo la mchungaji anayehusishwa na imani ya kishirikina hayajafukuliwa.

Watu wanne zaidi walikufa baada ya kugundulika wakiwa wana njaa kali katika kanisa la Good News International, wakiwa na waumini wenzao.

Polisi wameiomba mahakama kubakia na mchungaji huyo kwa muda zaidi, wakati uchunguzi wa vifo hivyo ukiendelea.

Mchungaji huyo aliwahi kukamatwa mara mbili mwaka 2019 na mwezi Machi mwaka huu, akihusishwa na vifo vya watoto na kuachiwa kwa dhamana wakati kesi zote mbili zikiendelea.