Hafla ya maombolezi kuiaga miili ya wanajeshi 14 wa Tanzania waliouawa katika shambulio la waasi wa ADFkatika eneo la Semuliki wilayani Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tarehe 7 Disemba zimefanyika mjini Beni leo kabla ya maiti hizo kusafirishwa kurejeshwa Tanzania.