Taarifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinasema majeshi ya Rwanda yamevuka mpaka na kuingia katika nchi hiyo kufanya uvamizi wa vijiji kadhaa katika wilaya ya Nyiragongo mapema leo. Msemaji wa jeshi la Congo ,mkoani Kivu ya Kaskazini, Meja Ndjike Kaiko amesema hali imerudi kuwa tulivu na raia wanaendelea na shughuli zao.