1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Milipuko miwili yautikisa mji mkuu wa Ukraine, Kyiv

11 Novemba 2023

Milipuko miwili mikubwa imeutikisa mji mkuu wa Ukraine, Kyiv leo asubuhi ikiwa ni tukio la hivi karibuni kabisa la kulengwa kwa mji huo baada ya wiki kadhaa za utulivu.

https://p.dw.com/p/4Yh9C
Wakaazi wa mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, wakiwa wamejihifadhi kwenye kituo cha treni kikimbia mashambulizi ya Urusi.
Wakaazi wa mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, wakiwa wamejihifadhi kwenye kituo cha treni kikimbia mashambulizi ya Urusi.Picha: Thomas Peter/REUTERS

Waandishi habari wa shirika la AFP wameripoti kuona moshi angani muda mfupi kabla ya kuanza kulia kwa ving´ora vya tahadhari ya mashambulizi ya anga.

Meya wa mji huo Vitali Klitschko ameandika kwenye ukurasa wa Telegram kuwa milipuko hiyo ilikuwa ni makombora yaliyoulenga mji huo lakini yalidunguliwa na mifumo ya ulinzi ya Ukraine.

Hakuna ripoti zozote za majeruhi kutokana na kisa hicho. Mji huo mkuu wa Ukraine umeshuhudia karibu wiki nane za utulivu licha kuendelea kwa vita upande wa mashariki.

Mnamo Spetemba 21 mifumo ya ulinzi ya Ukraine iliyotolewa kwa sehemu kubwa na mataifa ya magharibi ilidungua kombora moja ambalo mabaki yake yaliyoanguka yaliwajeruhiwa watu 7 mjini Kyiv.