Misri yatinga fainali AFCON
2 Februari 2017Matangazo
Lakini licha ya kutolewa Burkina Faso imejijengea sifa ya kuwa moja kati ya timu vigogo katika bara hilo, baada ya kukaribia kuingia katika fainali yake ya pili baada ya ile ya kwanza mwaka 2013 ambapo ilipoteza mchezo huo dhidi ya Nigeria. Mwenzangu Sekione Kitojo alipata fursa ya kuzungumza na mwandishi habari wa michezo David Kwalimwa aliyeko mjini Libreville na alimuuliza kuhusu tathmini yake kuhusu Burkina Faso na Misri.