Carol-Waithira Mühlenbrock alikulia nchini Kenya na kusoma chuoni huko. Alikuja Ujerumani miaka 17 iliyopita na kuanza upya kujenga maisha. Leo, yeye ni mmiliki wa mgahawa, mpishi mkuu na anaeneza mapishi yake pamoja na uzoefu wake kupitia mitandao ya kijamii. Katika video hii, anazungumzia jinsi alivyofikia mahali alipo leo na jinsi mtazamo wake kuhusu anachokiona kama “nyumbani” umebadilika.