Ndayishimiye amuondoa mkuu wa mamlaka ya ukusanyaji ushuru
6 Desemba 2024Matangazo
Jean Claude Manirakiza anatuhumiwa kuweka wazi upungufu wa kiwango cha mapato kinachokusanywa na taasisi hiyo katika kipindi cha miezi minne iliyopita. Afisa huyo alikaririwa akitoa matamshi hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya mlipa kodi mnamo Disemba 3.
Mabadiliko hayo kwenye uongozi wa taasisi ya kukusanya mapato ya serikali yametokea baada ya Mkuu wa Olucom shirika la kupambana na rushwa Gabriel Rufyiri kusema hivi karibuni kuwa taasisi hiyo OBR haiwezi kufanikisha majukumu yake kwa muda wote itasalia chini ya mamlaka ya rais.
Burundi inakabiriwa na hali tete kiuchumi mnamo miezi ya nyuma ambapo sarafu ya faranga imekuwa ikishuka thamani na kusababisha mfumuko wa bei za bidhaa.