1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa ANC wafunguliwa Polokwane

Oummilkheir16 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CcHM

Polokwane-Afrika kusini:

Mkutano mkuu wa chama tawala cha Afrika Kusini-African National Congress-ANC umefunguliwa mjini Polokwane.katika jimbo la Limpopo kaskazini magharibi ya nchi hiyo.Mkutano huo unapewa umuhimu mkubwa na unatazamiwa kuamua juu ya hatima ya kisiasa wa rais Thabo Mbeki.Hali ni tete na wajumbe zaidi ya elfu nne wa chama hicho kinachodhibiti uongozi wa Afrika kusini tangu enzi za ubaguzi wa rangi na mtengano zilipotoweka mnamo mwaka 1994,,wanabidi wamchague kiongozi wa chama kwa kipindi cha miaka mitano, uamuzi utakaoshawishi pia muundo wa serikali ya nchi hiyo yenye wakaazi milioni 48.Rais Thabo Mbeki anatetea tena wadhifa huo dhidi ya mpinzani wake mkubwa,makamo wa rais wa zamani Jacob Zuma.Hatima ya rais Thabo Mbeki itajulikana kesho.Katiba ya nchi hiyo haimruhusu rais Mbeki kutetea wadhifa wake wa urais kwa mara ya tatu