Chama tawala cha African National Congress, ANC, cha Afrika Kusini kimeanza leo kuwa na mkutano wake mkuu, huku rais wa nchi hiyo,Thabo Mbeki, akikiri kwamba mabalaa mawili ya umasikini na ukosefu wa nafasi za kazi bado hayajapatiwa dawa nchini humo, licha ya kwamba mafanikio mengi yamepatikana tangu chama hicho kuweko madarakani na kuporomoka mfumo wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994.
https://p.dw.com/p/CHBz
Matangazo
Pia alikiri kwamba haiwezekani kuyatanzua matatizo ambayo yamelimbikizwa mnamo miaka 350 kwa miaka 13 tu ya demokrasia.