1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele kati ya Korea mbili umeakhirishwa hadi October

18 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBY5

Seoul:

Mkutano wa kilele kati ya Korea mbili uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu,umeakhirishwa.Viongozi wa Korea ya kaskazini wameomba mkutano huo wa kilele uakhirishwe hadi mapema mwezi wa october mwaka huu.Ofisi ya rais wa Korea ya kusini iliyotangaza habari hizo imesema viongozi wa serikali ya mjini Pyongyang wameyataja maafa yaliyosababishwa na mafuriko ya hivi karibuni kama sababu ya kutaka mkutano huo wa kilele uakhirishwe.Kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu ,mafuriko hayo yamegharimu maisha ya zaidi ya watu 300 katika Korea ya kaskazini.