Mkutano wa kilele wa Korea
2 Oktoba 2007Rais Rah Moo Hyun wa Korea ya Kusini, mapema leo asubuhi, alivuka mpaka unaozitenganisha Korea mbili na kuingia mjini Pyongayang,mji mkuu wa Korea ya kaskazini. Roh Moo Hyun, aliuvuka mpaka huo kwa mguu na akaelezea matumaini kuwa siku moja utatoweka kabisa. Huu ni mkutano wapili tu wa kilele tangu nchi hii kugawika miaka 50 iliopita.
Katika mkutano wao wa kilele baina ya Roh wa Korea ya kusini na Kim Jong II wa Korea ya kaskazini,inatazamiwa kuzungumhia mfumo mpya wa amani kwa nchi hii iliogawika tangu 1953 kufuatia vita vya Korea.
Alipowasili rais wa Korea ya Kusini kwa mkutano huu wapili wa kilele tangu ule wa mwaka 2000,alilahkiwa na umati wa wakorea ya kaskazini uliomshangiria kwa kupepea maua mekundu na ya waridi akikaribishwa mikono miwili na mwenyeji wake Kim Jong II.Baada ya makaribisho hayo walikagua pamoja gwaride la kijeshi.
Picha kutoka sherehe hii ya makaribisho zilioneshewa moja kwa moja na timu ya wapigakamera kutoka Korea ya kusini iliofuatana na ujumbe wa rais kutoka Seoul, mji mkuu wa K. Kusini.
Rais Roh na Kim Yong II,wakati wa sherehe hizi za makaribisho hawakuwa na fursa ya kuzungumza sana.Pia viongozi wote wawili wakionekana na wasi wasi kidogo mbele ya mwenziwe.Baada ya dakika chache kila mmoja aliingia katika motokaa yake kuelekea kwenye jumba alikofikia mgeni wake.
Baada ya mazungumzo ya kwanza hii leo,rais Roh wa K.kusini atahudhuria burdani maalumu ya umma wa watu-maarufu kwa jina la Airang- na mnamo siku 2 zijazo, atazuru eneo maalumu la kiuchumi la Kaesong na kukutana huko mara kadhaa na kiongozi wa Korea ya kaskazini, Kim Jong II.Wananchi wa Korea ya kaskazini wanaipokeaje ziara hii na mkutano huu wa kilele ? Wao wamekuwa wakisitasita kama vile mmojawao anavyosimulia njiani:
“Natumainia kuungana tena kwa Korea wakati Fulani.Lakini, siaamini kuwa rais huyu ana uwezo wa kufikia shabaha hiyo.Rais wa sasa amewapa watu matumaini mengi ambayo hayatatimizwa.Hata wanaofanya kazi nao ni walarushua.”
Matamshi kama hayo mtu aweza kuyasikia sana katika mitaa ya mji mkuu Seoul wa K.kusini.Wakorea wamevunjwa moyo na miaka iliopita ya serikali hii ya Korea ya kusini na wanauangalia mkutano huu wa kilele kati ya viongozi hawa 2 wa Korea ni kama tafrija tu ya kufurahisha moyo.
Rais wa K.Kusini Roh ,ana muda wa miezi 4 tu madarakani na baadae raias mpya atabidi kuamua usuhuba na hasimu Korea ya kaskazini uchukue umbo gani.