Mkutano wa kilele wa mataifa ya Afrika kufanyika Addis
15 Novemba 2018Matangazo
Viongozi wa Afrika wanatarajiwa kuwasili mwishoni mwa juma hili mjini Addis Ababa kwa ajili ya mkutano maalum wenye lengo la kupitisha mageuzi yaliyokuwa yakijadiliwa kwa muda mrefu katika Umoja huo wa Afrika.
Mabadiliko yanalenga kuuboresha na kuuwezesha Umoja wa Afrika - ambao ni wito wenye nguvu kwa umoja huo ambao mara nyingi unaonekana kuwa usiyo na uwezo na unaotegemea zaidi wafadhili, na wadadisi wanasema muda wa kupatikana makubaliano ni mfupi.
Mkutano huo maalum utafanyika katika makao makuu wa Umoja huo mjini Addis Ababa Jumamosi na Jumapili kwa msisitizo wa rais wa Rwanda Paul Kagame, ambaye ndie yuko nyuma ya mageuzi hayo.