Mkutano wa kuhusu vita Mashariki ya Kati waanza mjini Cairo
21 Oktoba 2023Katika hotuba yake Al-Sisi amesema ameitisha mkutano huo kutafuta makubaliano ya njia za kumaliza hali mbaya ya kiutu kwenye Ukanda wa Gaza na kufufua mchakato wa kusaka amani kwa mzozo kati ya Israel na Wapalestina.
Jordan yasema kuwalazimisha wapalestina kuondoka katika makazi yao ni makosa ya uhalifu wa kivita
Akihutubia mkutano huo Mfalme Abdullah wa Jordan amesema kuwalazimisha wapalestina kuondoka kwenye makaazi yao au kuwafanya kuwa wakimbizi wa ndani yatakuwa makosa ya uhalifu wa kivita.
Soma pia: HRW yaituhumu Magharibi kwa unafiki juu ya Gaza
Mkutano huo wa leo unahudhuriwa na viongozi wengi wa mataifa ya kiarabu na wawakilishi kutoka mataifa kadhaa ya magharibi pamoja na China. Marekani iliyo mshirika muhimu wa Israel haijatuma mwakilishi wake hali inayozusha mashaka kuhusu mafanikio ya mkutano huo wa Cairo.