Mkutano wa pande sita kuhusu Korea Kaskazini
23 Novemba 2007Matangazo
Majadiliano ya pande sita kuhusika na mradi wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini huenda yakaanza upya katika kipindi cha majuma mawili yajayo. Urusi imeshakubali kushiriki katika duru mpya ya majadiliano kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba. Majadiliano yaliyopendekezwa na China hasa yatashughulikia hatua za kufuatiliza katika utaratibu wa kubomoa kiwanda cha kinyuklia cha Korea ya Kaskazini.
Mapema mwezi huu,Korea ya Kaskazini,chini ya usimamizi wa wakaguzi wa Marekani,ilianzisha harakati hizo kwenye kiwanda cha nyuklia cha Yongbyon.