Mkutano wapili wa kilele Korea
2 Oktoba 2007Mkutano wa kwanza kabisa kati ya Korea mbili tangu kupita miaka 7 ulianza leo kwa shangwe za maalfu ya wakorea ya kaskazini waliomkaribisha rais Roh Moon-hyun wa Korea ya Kusini, mjini Pyongayang.
Mkutano huu hadi sasa una kasoro ya mazungumzo ya kina juu ya hatima ya korea.
“Nimefurahi kuonana nawe”-hayo tu ndio maneno aliosikika akisema hadharani Kiongozi wa Korea ya kaskazini Kim Jong Il akimwambia mgeni wake.
Mkutano wa leo, ni wapili tu tangu Korea kugawanywa mapande 2 kufuatia vita vya pili vya dunia.Kiongozi wa Korea ya kaskazini Kim hakuruhusu mkutano zaidi na mgeni wake Roh na badala yake amemtupia jukumu la kumshughulikia makamo wake Kim Yong Nam.Kim hakuonesha ubashasha wowote alipomkaribisha mgeni wake alievuka mstari wa mpaka unaozigawa Korea mbili kwa mguu.
Tabia alioionesha leo Kim ni tofauti kabisa na pale alipomkaribisha rais wa zamani wa Korea ya Kusini Kim dae-jung katika mkutano wa kwanza wa kilele kati ya Korea mbili.
Wakorea ya kaskazini waliofika mpakani kwa umati mkubwa wakipepea maua yao ya sandarusi ya rangi nyekundu na waridi.
Rais wa korea ya Kusini hatahivyo, alifurahia msafara wake katika motokaa isio na kipaa akipiota katika barabara za Pyongyang na makamo wa K.kaskazini Kim Yong-nam.Barabara za jiji hilo la Pyongyang lilipambwa mapambamo mbali mbali ya rangi-rangi.
Ziara hii ya siku 3 ya rais wa Korea ya kusini imefanyika huku mazungumzo ya kimkoa yakiendelea kuishawishi Korea ya kaskazini kuachana kabisa na mradi wake wa silaha za kinuklia ili ipewe misaada mingi na nchi za magharibi pamoja na kutotengwa kama nchi ilioapizwa.
Na wakati mkutano wa kwanza hapo 2000 ulioangaliwa ni tokeo muhimu la kihistoria lililoongoza kupunguza mvutano kati ya Korea mbili,mkutano huu wa sasa wa kilele haukushangiriwa mno hivyo.
Mkorea mmoja alieleza:
“Nina matumaini kuw siku moja Korea itaungana tena.Lakini,sidhani kuwa rais huyu wa Korea ya kusini atatimiza matarajio hayo.”
Haikusaidia kuwa mkutano wapili bado unafanyika Pyongyang licha ya kuwa iliafikiwa hapo 2000 kuwa Kim Jong-il angekwenda nae Seoul,mji mkuu wa korea ya kusini kwa mkutano huu wapili.
Wakosoaji wa rais Roh wa Korea ya kusini, wamtuhumu kwamba anaitumia ziara hii kupalilia ndoto za kuungana tena Korea ili kuimarisha nafasi za chama chake cha ki-liberali kiliopo nyuma katika uchunguzi wa maoni kwa uchaguzi wa rais wa hapo desemba.Roh kikatiba hawezi kugombea tena.
Mazungumzo ya kwanza rasmi kati ya viongozi wa Korea hizi 2 yanatazamiwa hasa kufanyika kesho kabla ya rais Roh kurejea seoul,keshokutwa alhamisi.