1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa WHO atoa mwito kwa Israel kusitisha mashambulizi

30 Desemba 2024

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus ametoa mwito kwa vikosi vya Israel kusitisha mashambulizi yanayolenga hospitali katika ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4ogVB
Deutschland Berlin | World Health Summit | WHO-Generaldirektor Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus akiwahutubia washiriki wa Mkutano wa Kilele wa Afya Duniani wa 2024 mjini Berlin Oktoba 14, 2024. Picha: John Macdougall/AFP/Getty Images

Ametoa wito huo baada ya hospitali katika eneo hilo kushambuliwa hivi karibuni.Akiandika katika mtandao wa X zamani Twitter, Kiongozi huyo amesema hospitali katika ukanda wa Gaza kwa mara nyingine zinakabiliwa na mashambulizi na mifumo ya afya inatishiwa kwa kiwango kikubwa. Hapo jana, watu saba waliuawa baada ya jeshi la Israel kuishambulia hospitali ya Al wafa huko Gaza kwa mujibu wa shirika la kipalestina la ulinzi wa kiraia.Vikosi vya Israel pia viliwashikilia zaidi ya Wapalestina 240 wakiwemo wafanyakazi kadhaa wa hospitali ya Kamal Adwan siku ya Ijumaa, miongoni mwao ni mkurugenzi wa hospitali hiyo Hussam Abu Safiya, taarifa hizo ni kwa mujibu wa mamlaka ya afya ya Gaza inayosimamiwa na Hamas. Jeshi la Israel limesema linawalenga wanamgambo wa Hamas katika mashambulizi hayo na kwamba wanayatumia majengo ya hospitali kama sehemu ya maficho.