Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo, MONUSCO kinarefusha muda wake wa kubakia mashariki mwa nchi hiyo, kufuatia kile waziri wa mambo ya nje wa Kongo, Therese Kayikwamba alichosema kuwa bado taifa hilo lina changamoto ya kiusalama. Amina Abubakar amezungumza na mwanaharakati wa Lucha, shirika la kiraia lililotaka MONUSCO iondoke Kongo.