MOSCOW: Rais Putin aionya jamii ya kimataifa kuhusu Korea Kaskazini
25 Oktoba 2006Matangazo
Rais wa Urusi, Vladamir Putin, ameionya jamii ya kimataifa dhidi ya kuishinikiza Korea Kaskazini ikiwa inataka kuutanzua mzozo wa nyuklia wa nchi hiyo.
Akizungumza wakati wa mahojiano yake kwenye runinga ya kitaifa, rais Putin amesema jaribio la zana za kinyuklia la Korea Kaskazini haliwezi kukubalika.
Hata hivyo rais Putin amesema serikali ya Pyongyang iliamua kufanya jaribio lake mnamo Oktoba 9 kwa sababu wasuluhishi katika mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini walishindwa kukubaliana.
Rais Putin amesema ataendelea kuwa na mamlaka nchini Urusi hata baada ya kuondoka madarakani mwaka wa 2008, kwani sheria haimruhusu kugombea wadhifa wa uraisi kwa mara ya tatu.