1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi: Ukraine ilijaribu kuharibu daraja la Crimea

12 Agosti 2023

Wizara ya Ulinzi ya urusi imesema Ukraine hii leo ilijaribu kulishambulia daraja muhimu kwenye rasi ya Crimea kwa kutumia kombora chapa S-200 lakini haikufanikiwa na kwamba hakuna uharibifu wowote uliotokea.

https://p.dw.com/p/4V682
Daraja la Crimea
Daraja la CrimeaPicha: Alexander Nemenov/AFP

Taarifa iliyochapishwa na wizara hiyo imesema kombora hilo la Ukraine lilibainika mapema na kudunguliwa na mifumo ya ulinzi ya Urusi kabla ya kufanya uharibifu kwenye daraja la Crimea linalokatisha ujia wa maji wa Kerch.

Soma zaidi: Urusi na Ukraine zahujumiana kwa droni na makombora

Daraja hilo lenye urefu wa kilometa 19 linaiunganisha Urusi na rasi ya Crimea ambayo Moscow iliinyakua kwa mabavu kutoka Ukraine mwaka 2014. Ukraine imekuwa ikililenga daraja hilo tangu Urusi ilipoivamia nchi hiyo mwanzoni mwa mwaka uliopita.

Mapema hii leo Urusi ilisema kwamba pia imefanikiwa kuzima shambulio jingine la Ukraine dhidi ya rasi ya Crimea kwa kuzidungua ndege 20 zisizo na rubani. Ukraine yenyewe haijasema chochote kuhusu madai hayo.