1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpango mpya wa bima ya afya

Hamidou, Oumilkher6 Oktoba 2008

Wakuu wa vyama vinavyounda serikali kuu ya mungano wakutana leo hii mjini Berlin

https://p.dw.com/p/FUnV
Bundeskanzlerin Angela Merkel lacht am Montag, 22. Sept. 2008, beim Unternehmertag der CDU/CSU Bundestagsfraktion in Berlin. Die Teilnehmer hatten dabei auch Gelegenheit, der Kanzlerin Fragen zu stellen. (AP Photo/Miguel Villagran) --- German Chancellor Angela Merkel smiles during the entrepreneurs day of the joint faction of the CDU/CSU parties in Germany's parliament, in Berlin, Germany, on Monday, Sept. 22. 2008. (AP Photo/Miguel Villagran)Picha: AP



Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha zaidi na malumbano ya nani awe kiongozi wa chama cha Christian Social Union-CSU,mpango wa malipo ya aina moja kwa walipa bima ya afya katika mashirika ya serikali na jinsi serikali za Umoja wa ulaya zinavyopanga kukabiliana na mzozo wa fedha.


Kwanza lakini tuelekee Bavaria ambako gazeti la WELT am Sonntag linaulinganisha mzozo wa kuania uongozi ndani ya chama cha CSU na laana.Gazeti linaendelea kuandika:


Kwamba chama tawala kinaporomoka namna hiyo,haitokani pekee na mwanya kati ya maadili ya kale na yale ya kimambo leo.Sababu hasa ni kwamba chama hicho cha CSU kinashindwa kuwakilisha ipasavyo na kwa namna ya kuaminika, masilahi ya wapiga kura wa aina zote; naiwe wahafidhina,au  ya watu walioachana,waliokwenda nje ya ndowa,wanaolea watoto peke yao au hata wapiga kura mahanithi.CSU kimeanza kujirekebisha,na kwa namna hiyo kinapoteza sifa zake kama chama cha Bavaria.Hakihubiri tena kama ndugu zao wa CDU walivyokua wakipenda kusikia katika jengo lao la Konrad Adenauer Haus.Mshikamano ni muhimu sawa na kujiambatanisha na wakati kulivyo muhimu" .


Hayo ni maoni ya Die Welt am Sonntag. Yanalingana na yale yaFRANKFURTER ALGEMEINER ZEITUNG linaloandika:



Kutokana na hali namna ilivyo,ufumbuzi ni mmoja tuu. Horst Seehofer.Yeye ndie anaestahiki kuiokoa jahazi isizame.Hata jahazi ya Bavaria,aachiwe yeye usukani.Huo lakini si ufumbuzi wa maana,si kwa CSU na wala si kwa CDU.Kwasababu kwakua  CSU ni chama cha Bavaria,kinabidi kisalie vivyo hivyo ili kuweza kuimarisha uzito wake katika daraja ya kitaifa na katika medani ya siasa za shirikisho.Huo tuu ndio ufumbuzi unaoingia akilini kwa sasa.Seehofer lakini anaweza pia kujibwaga katika asiasa za kimkoa tuu,ingawa muhimu zaidi kwa chama cha CSU kwa sasa ni kuendelea kusaka wezani sawa utakaopelekea kupatikana uongozi badala ya kuzidi makali mivutano.



Gazeti la BERLINER MORGENPOST linazungumzia mpango wa serikali wa kuanzisha malipo ya aina moja ya bima ya afya ya mashirika yanayomilikiwa na serikali.Gazeti linaendelea kuandika:



Pengine mpango huo ungewavutia wanchi wengi tuu.Kwasababu afya ni jambo muhimu kwa maisha yao.Lakini wanasiasa,matabibu,wawakilishi wa mashirika ya bima ya afya na wakuu wa hospitali wamekua daima wakiuweka kando mjadala kuhusu suala hilo.Wanahisi labda ni kazi nyingi kuwafafanulia wananchi mpango wa marekebisho utakaokua na faida kwao.Wanaona bora kuzozana hadharani,kiasi gani wananchi wanabidi wawalipe.Hali hiyo inatisha.Seuze tena kuna dhana ,mpango wa mashirika ya bima yanayomilikiwa na serikali wa kubuni fuko la afya,umelengwa kukusanya fedha tuu ili kukabiliana na kishindo kitakachofuatia baadae.




Gazeti la BILD Am Sonntag  linamulika mkutano wa leo mjini Berlin,na kuendelea kuandika:



Wakuu wa vyama ndugu vya CDU/CSU na wale wa SPD watakapokutana hii leo katika ofisi ya kansela mjini Berlin,mada kuu watakayopizungumzia ni kuhusu ahadi za serikali kuu ya muungano:Nayo ni kupunguza kiwango cha kodi ya mapato kwa chini ya asili mia 40.Kwasababu kwa kuongezwa kiwango cha malipo ya bima ya afya na kupunguza mchango wa bima ya wasiokua na kazi pekee haitoshi.Kwa hivyo ni vyema kama kansela ataitanabahisha serikali yake ikubali fedha za kugharimia nyongeza za bima ya afya zitokee mahala pengine.Na matamshi yake yafuatwe kivitendo-sio tuu leo jioni katika ofisi ya kansela,bali hata siku zijazo katika bunge la shirikisho.