SiasaRwanda
Mshukiwa wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda, mahakamani
10 Mei 2023Matangazo
Philippe Hategekimana, mwenye umri wa miaka 66 ambaye alipata uraia wa Ufaransa chini ya jina la Philippe Manier, atashitakiwa katika mahakama ya Paris kwa mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinaadamu. Atakuwa mtu wa karibuni kabisa kufunguliwa mashitaka nje ya nchi kuhusiana na mauaji ya karibu watu 800,000. Hategekimana anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya Watutsi na pia kuweka vizuizi barabarani ili kuwazuia Watutsi ambao baadae waliuawa katika mkoa wa kusini wa Nyanza, ambako alifanya kazi kama afisa mwandamizi wa polisi. Amekanusha madai hayo. Hiyo ni kesi ya tano ya aina hiyo nchini Ufaransa kuhusiana na mauaji ya kimbari Rwanda.