Nchini Tanzania wakati mjadala kuhusu azimio la serikali ya nchi hiyo juu ya makubaliano kati ya serikali ya Tanzania na kampuni ya kimataifa ya DP World ya Dubai ya uendeshaji wa bandari ya Dar es salaam ukipamba moto, Spika wa bunge Tulia Ackson amesema bunge la nchi hiyo bado halijaamua chochote juu ya jambo hilo na kuwambia wananchi waendelee kutoa maoni.