1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muaji wa kimbari akamatwa Gabon

20 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEZK

Dar es Salaam:

Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za mauaji ya kimbari nchini Rwanda ya mwaka 1994 imetangaza kukamatwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Stesheni ya Redio iliyokuwa inachochea mauaji hayo. Mahakama ya ICTR imetangaza mjini Arusha, Tanzania kuwa Joseph Serugendo, aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Stesheni ya Redio na Televisheni ya Mille Collines (RTLM) amekamatwa nchini Gabon. Redio RTLM inajulikana sana kwa kuchochea mauaji ya „Mende“ kama vile Watutsi walivyokuwa wakiitwa wakati wa mauaji hayo ya kimbari ya watu 800,000. Mahakama pia imetangaza kuanzishwa kwa kesi za waliokuwa Maafisa wanne. Watu hao ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Edouard Karemera; aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Madini, Joseph Nzirorere na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, Mathieu Ngirumpatse.