1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muda wa tume ya umoja wa mataifa nchini Burundi warefushwa kwa miezi sita

1 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF8A

New-York:

Kwa upande mwengine baraza la ausalama la umoja wa mataifa limerefusha kwa miezi sita shughuli za tume ya umoja wa mataifa nchini Burundi.Azimio la baraza la usalama limeungwa mkono na wanachama wote 15..Azimio hilo linasifu mipango ya kuitishwa uchaguzi kuambatana na makubaliano ya amani ya Arusha.Uchaguzi mkuu,awamu ya mwanzo ikiwa uchaguzi wa mabaraza ya miji utakaoanza ijumaa ijayo,unatarajiwa kukamilisha utaratibu wa amani ulioingia njiani baada ya miaka 12 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi hiyo ndogo ya Afrika kati.Tume ya Umoja wa mataifa nchini Burundi ONUB imeundwa mwezi June mwaka jana na inawaleta pamoja wanajeshi 5378,askari polisi 102 na rais wengineo 327.