1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MUMBAI/INDIA :idadi ya waliouawa katika mashamblio ya kigaidi yavuka 160

12 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG8L

Idadi ya watu waliouawa katika mashambulio ya mabomu mjini Mumbai, nchini India sasa imevuka 160.

Watu wengine zaidi ya mia mine walijeruhiwa katika mashambulio hayo.

Maafisa wa serikali ya India wamearifu kuwa mabomu yapatayo saba yaliripuka ndani ya treni zilizokuwa zimejaa wasafiri.

Habari zinasema kuwa mashambulio hayo katika mji huo muhimu kiuchumi yalifanyika kwa uratibu wa hali ya juu.

Kutokana na hali hiyo India imechukua hatua za tahadhari za juu kwenye miji mingine mikubwa ya nchi hiyo.

Ingawa hadi sasa hakuna habari zozote juu ya watu ama makundi yaliyofanya muaaji hayo,inatuhumiwa kwamba wapiganaji wa Kashmir wametanda ugaidi huo.

Juhudi za kuwasaidia watu walioathirika kutokana na mashambulio hayo zinaendelea.

Viongozi kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamelaani unyama huo sambamba na kutoa mkono wa rambirambi .

Rais George Bush wa marekani ameyalani vikali mashambulio hayo na kusema kuwa mauaji ya watu wasiokuwa na hatia hayawezi kuhalalika.

Rais Bush ameeleza kuwa matendo hayo yanapaswa kuimarisha dhamira ya watu duniani kote juu ya kusimama pamoja na kupambana na ugaidi.

Viongozi wa Pakistan pia wamelaani unyama huo.