MUMBAI: Mvua kubwa yaendelea kuzusha hofu India
31 Julai 2005Matangazo
India imewaonya wakaazi wake kubakia majumbani mwao wakati mvua kubwa imeanza kunyesha tena katika eneo la mji wa Mumbai na maeneo ya karibu yaliyokumbwa na mafuriko mabaya zaidi wiki iliyopita.
Shughuli za kuusafisha mji na maeneo yaliyoathirika pamoja na kusambaza vyakula zimetatizwa kutokana na kuanza upya kwa mvua hiyo asubuhi ya leo.
Maafisa wa safari za ndege wametoa amri kwa mashirika ya ndege mjini Mumbai kufutilia mbali safari za ndege kutokana na hatari ukungu.
Taarifa zaidi zinasema idadi ya watu waliokufa kutokana na mvua hiyo huenda ikafikia 1000.