MUMBAI:Kansela Merkel amaliza ziara nchini India
1 Novemba 2007Matangazo
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amemaliza ziara ya siku nne nchini india kwa kusema kuwa ziara hiyo imeinua kiwango cha uhusiano baina ya nchi mbili hizo.
Akizunguzmza na waandishi habari mjini Mumbai bibi Merkel ameshauri haja ya Ujerumani na India kushirikiana zaidi kisiasa na kiuchumi.
Juu ya India , bibi Merkel amesema harakati za kupambana na umasikini bado ni changamoto kubwa kwa nchi hiyo.
India na Ujerumani zimetiliana saini makubaliano ya kupanuza ushirikiano katika sayansi,biashara na siasa.