Muramuya, Burundi. Kiongozi wa zamani wa waasi wa Kihutu kuwa rais wiki ijayo.
13 Agosti 2005Kiongozi wa zamani wa waasi wa Kihutu ambaye ana hakika ya kuwa rais mpya wa Burundi baada ya kipindi cha mpito wiki ijayo ametoa tamko la kujivua nafasi ya kiongozi wa wapiganaji wa chini kwa chini jana.
Pierre Nkurunziza, kiongozi wa majeshi ya chama cha Forces for the Defence of Democracy, FDD, ambayo yamevunjwa rasmi mbele ya wajumbe wa jeshi rasmi la nchi hiyo kabla ya uchaguzi wa hapo August 19 wa rais mpya wa nchi hiyo utakaofanywa na bunge ambapo atakuwa mgombea pekee.
Yeye pamoja na wapiganaji wenzake 40 wa zamani, ikiwa ni pamoja na maafisa kadha wa ngazi ya juu katika tawi la kisiasa la chama cha FDD, ambacho kimepata ushindi katika chaguzi mbali mbali na kumhakikishia Nkurunziza ushindi, wameshiriki katika sherehe hizo katika eneo la kati la Burundi.