Mkuu wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin na maafisa wake 6 wa ngazi za juu wameuwawa kwenye ajali ya ndege iliyoanguka, kaskazini mwa Moscow. Wagner wenyewe wanadai ndege hiyo imedunguliwa. Je tukio hili linatowa mwelekeo gani wa mustakabali wa kundi hilo? Msikilize Saumu Mwasimba akizungumza na Mohammed Abdul-Rahman, mchambuzi wa siasa za kimataifa aliyewahi kuishi Urusi.