1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano wa India na Pakistan waendelea

7 Desemba 2008
https://p.dw.com/p/GB1U
New Delhi:
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa India amesema kwamba ripoti za Pakistan kuhusu simu iliopigwa na mtu aliyejifanya ni waziri huyo wakati wa mashambulio ya hivi karibuni mjini Mumbai, ni jaribio la kujiondoa kwenye lawama.Simu hiyo aliyopigiwa Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari na mtu aliyedai ni Waziri wa mambo ya nchi za nje wa India Pranab Mukherjee, ilisababisha Pakistan kuwa katika hali ya tahadhari dhidi ya hujuma ya kijeshi kutoka India, wakati wanaharakati wa Kiislamu walikua wakipambana na majeshi ya usalama mjini Mumbai. Magazeti nchini Pakistan yaliripoti jana kwamba mtu huyo alimwambia Bw Zardari kwamba India itachukua hatua ya kijeshi ikiwa Pakistan haitowakabidhi walioko nyama ya mashambulio hayo. Watu 172 waliuwawa katika mashambulio hayo kwenye maeneo kadhaa mjini Mumbai.
Katika taarifa yake,Waziri wa mambo ya nchi za nje wa India amesema kwamba hakupiga simu yoyote na akaelezea wasi wasi wake kwamba Pakistan inaweza kuzingatia kuchukua hatua ya tahadhari, kwa misingi ya simu ya udanganyifu kama hiyo ambayo Pakistan binafsi ilifafanua baadae kuwa ilikua ni ya uongo.