Mwaka mmoja tangu Tsunami kuipiga Somalia
19 Desemba 2005Ukanda wa mwambao wa Somalia, ukiwa umbali wa kilomita 4,500 kutoka kiini cha tetemeko hilo la ardhi chini ya Bahari, ulivurugwa na gharika hiyo. Idadi ya watu walioangamia kwenye Tsunami hiyo katika nchi hiyo iliokumbwa na vita vya kienyeji na michafuko haitojulikana. Janga hilo liliviangamiza vijiji vizima, kuzikatalata vipande vipande ngarawa na kuziangusha chini nyumba. Watu walipoteza mali na misingi yao ya maisha.
Somalia na Tsunami zitakuwa na maandishi ya herufi ndogo katika vitabu vya historia. Ukilinganisha na watu wengi waliokufa kutokana na uharibifu mkubwa uliojiri katika Bara la Asia, idadi ya watu waliopoteza maisha na kiwango cha uharibifu uliofanyika katika Pembe ya Afrika ni mdogo.
Jumuiya za kutoa misaada zinakadiria hadi watu 300 wamekufa katika mwambao wa eneo hilo wenye urefu wa kilomita 650, na karibu ya watu wengine 33,000 wameathirika moja kwa moja na balaa hilo. Lakini , kwa Somalia ambayo tangu hapo ipo katika hali ngumu, athari za Tsunami kwa nchi hiyo zilikuwa kubwa. Baada ya kuweko kipindi kirefu cha ukame, kulitokea mafuriko yaliosababishwa na mvuwa kubwa, mafuriko ambayo watu hawajaweza kuyasahau kutokana na uharibu iliofanyika. Kuengeza na hayo tena likaja balaa la Tsunami la Disemba 26.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Vyakula Duniani, WFP, kutokea Nairobi, lilikuwa shirika la mwanzo la misaada kuwasili katika eneo hilo la janga. Leo van der Velden, makamo wa mkurugenzi wa WFP katika Somalia, aliielezea hivi hali ya mambo katika eneo la Puntland, eneo lenye utawala wake wenyewe katika kaskazini mashariki ya Somalia, ilivokuwa mwaka mmoja uliopita:
Insert. O-Ton van der Velden…
+Sehemu ilioathirika sana ni ile ya Harfun, ambako maji ya baharini yalifurika kabisa. Majumba yaliharibika na misingi ya maisha ya watu, ngarawa zao na vifaa vya kuvulia vyote vilikumbwa na mafuriko. Maisha yao yalikuwa hatarini kwa vile kutokana na Tsunami, msimu wao wa kuvuwa samaki ulimalizika mapema; kwa kawaida huwa baina ya miezi ya Novemba na Mei.+
Wavuvi wengi ambao wakati huo walikuwa baharini na boti zao, hawajarejea tena majumbani. Mawimbi hayo makali ya bahari sio tu yaliviangamiza vijiji vizima, lakini pia miundo mbinu iliokuwa tangu hapo mibaya. Jumuiya za kimataifa zilitumia meli na pia magari makubwa ya mizigo, baada ya njia kutengenezwa, kusafirishia vyakula, madawa na mablangeti katika eneo hilo. Licha ya hali hiyo ngumu, misaada ya mwanzo iliwafikia watu walioathirika saa kumi baada ya kutokea balaa hilo. Leo van der Velden alikuwa pamoja na Shirika la WFP mahala hapo:
Insert: O-Ton van der Velden
+Naamini watu walifurahi sana pale Shirika la kuwahudumia watoto duniani, UNICEF, na Shiria la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Vyakula Duniani, WFP, tangu mwanzo yalituma misaada ya mwanzo na mpaka sasa yanasaidia. Watu hao wanatambua kwamba hawatasahauliwa, kwa vile msaada wa kujenga maisha mepya unahitajika kwa muda mrefu.+
Licha ya WFP na UNICEF katika eneo hilo pia yanafanya kazi shirika la Makaazi Duniani, Habitat, pamoja na yale yasiokuwa ya kiserekali katika Somalia, kama vile Jumuiya ya Kiislamu ya Misaada, katika kujenga nyumba, shule na kuirejesha miundo mbinu. Jumuiya hizo zimesaidia kutengeneza boti na kuwapatia wavuvi vifaa vipya. Wavuvi wa Kisomalia wanahitaji kusaidiwa kuondokana na woga walioupata wa kutotaka kwenda baharini kutokana na ile gharika ya Tsunami.. Maisha yao yanategemea kuvua papa na kamba ambao wanawasafirisha hadi Dubai. Leo van der Velden anaelezea hivi hali ilivyo sasa:
Insert: O-Ton van der Velden…
+Hivi sasa tayari msimu wa uvuvi umeanza. Kuna habari kwamba tangu kutokea Tsunami ya mwaka jana, kuna upungufu mkubwa wa uvuvi wa samaki na kamba, na kwamba kuna kamba wadogo zaidi kuliko hapo kabla. Lakini tunataraji hali ya mambo itakuwa bora.+
Wananchi katika maeneo yalioathirika hadi sasa wasitaraji msaada kutoka serekali kuu yao. Bado wababe wa kivita wenye nguvu ndio walio na usemi na wao wanajaribu kuhakikisha kwamba mamlaka yao yanakuwa salama.