Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Jumanne (02.04.2019) alikamilisha mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani. Aliingia madarakani mwaka uliopita akichukua mikoba ya uongozi baada ya mtangulizi wake waziri mkuu wa wakati huo, Hailemariam Desalegn, kujiuzulu kufuatia miaka miwili ya maandamano ya kuipinga serikali. Je, yapi ameyafanikisha?