1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanadiplomasia wa Marekani kukagua kinu cha nuklia Pyongyang

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVt9

SEOUL.Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani katika mzozo wa nuklia wa Korea Kaskazini anaelekea nchini humo kukagua kazi inayoendelea ya kufunga kinu kikubwa cha nuklia.

Ubalozi wa Marekani mjini Seoul Korea Kusini umesema kuwa mwanadiplomasia huyo Christopher Hill anatarajiwa kukagua kazi ya kukifunga kinu cha Yongbong kilichoko kaskazini mwa mji mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang.