Mwanaharakati maarufu Misri ahukumiwa miaka 5 jela
20 Desemba 2021Matangazo
Watu wengine wawili pia wamehukumiwa kwenda jela miaka 4.
Kwa mujibu wa dada wa mwanaharakati huyo, Mona Seif, Abdel Fattah, wakili wake Mohammed al Baqer na mwanablogu Mohammed Ibrahim kwa jina maarufu, ''Oxygen'' walishtakiwa kwa tuhuma za kutoa habari za uwongo katika kesi iliyoendeshwa katika mahakama ya mjini Cairo.
Wote watatu wamekuwa wanazuiliwa mahabusu tangu mwaka mwezi Septemba mwaka 2019.
Aidha Abdel Fattah ambaye ni mwanaharakati maarufu katika vuguvugu la mwaka 2011 lililomuondowa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak baada ya kukaa madarakani miongo mitatu aliwahi huko nyuma kufungwa miaka mitano jela.