Mwandishi wa Habari wa Radio Okapi auwawa mjini Bukavu,DRC
24 Novemba 2008Matangazo
Itakumbukwa kuwa ni mara ya pili kwa kitendo cha namna hii kutokea katika kipindi cha miezi 18.Kituo cha redio cha Okapi kilianzishwa kwa minajili ya kuimarisha juhudi za kumaliza vita vinavyozonga Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Ili kupata picha kamili Thelma Mwadzaya alizungumza na Jerome Sekana mwanachama wa chama cha waandishi wa habari wa Kongo UNPC aliye pia msimamizi wa kituo cha redio cha Raga FM.