1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwili wa mwanamke aliyebakwa kurejeshwa India

29 Desemba 2012

Mwili wa mwanamke wa India ambaye amefariki hospitalini nchini Singapore baada ya kubakwa kinyama mjini New Delhi utarejeshwa kwa ndege maalum ya kukodi baadaye leo Jumamosi(29.12.2012).

https://p.dw.com/p/17AyM
epa03519152 Indian protesters and commuters light candles during a protest campaign by Youth Congress against the gang rape of a student last week, in Calcutta, India, 28 December 2012. The 23-year-old Indian gang rape victim being treated in a Singapore hospital was in extremely critical condition and struggling to survive, doctors said on 28 December. The woman was raped and beaten in a moving bus in New Delhi on 16 December. The attack triggered protests in the Indian capital and other cities. EPA/PIYAL ADHIKARY +++(c) dpa - Bildfunk+++
Waombolezaji wakiweka mishumaaPicha: picture-alliance/dpa

Balozi  wa  India  nchini  Singapore T.C.A Raghavan  amewaambia waandishi  habari, saa  kadha  baada  ya  mwanamke  huko  kufariki kutokana  na  viungo  vyake  kushindwa  kufanya  kazi  katika hospitali  nchini  Singapore  ambako  alikuwa  akipatiwa  matibabu.

Mwanamke  huyo  na  ndugu  wa  marehemu  watasafirishwa kwenda  India   katika  ndege  maalum  ya  kukodi  baadaye  mchana wa  leo  Jumamosi, (29.12.2012) , amesema  Raghavan.

Waziri mkuu  ahuzunika

Waziri  mkuu  wa  india  Manmohan Singh  amesema   kuwa amesikitishwa  sana  na  kifo  cha  mwanamke  huyo  ambaye alifanyiwa  vitendo  vya  kinyama  kwa  kubakwa  na  kundi  la  vijana na  kwamba  maandamano  yaliyozuka  kutoka  na  kitendo  hicho , "yanaeleweka".

epa03518670 An Indian protester holds a candle and others placards, during a silent protest march held by sex workers, transgender and gays, against the gang rape of a student in New Delhi a week back, in Mumbai, India, 27 December 2012. The 23 year old woman who was gang-raped by 6 men on a moving bus on the night of 16 December 2012 has been flown to a Singapore hospital for further treatment of her severe internal injuries. EPA/DIVYAKANT SOLANKI
Wanawake wakiandamana nchini India wakipinga matumizi ya nguvu katika ngonoPicha: picture-alliance/dpa

"nimesikitishwa  mno  kufahamu  kuwa  mhanga  huyo  wa mashambulizi  ya  kinyama  ambayo  yalifanyika  Desemba 16  mjini New Delhi  ameshindwa kunusurika  kutokana  na  majeraha makubwa  aliyoyapata  baada  ya  shambulio dhidi  yake, " ameandika  waziri  huyo  mkuu  katika  tovuti  yake.

"Tumekwisha  ona  hisia  na  nguvu  ambazo  tukio  hili limesababisha. Hii  ni  hali  ambayo  inaeleweka  kutoka  kwa  vijana wa  india  ambao  wanataka  mabadiliko  ya  kweli.

"Nataka  kuwaambia , familia  yake  na  taifa  kwa  jumla  kuwa amepoteza maisha,  ni  juu  yetu  wote  kuhakikisha  kuwa  kifo chake  hakitakuwa  cha   bure."

Indian Prime Minister Manmohan Singh attends a Full Planning Commission meeting at his residence in New Delhi on September 15, 2012. Indian Prime Minister Manmohan Singh defended September 15 a string of economic reforms unveiled by his government, despite protests over higher fuel prices and new foreign investment rules. AFP PHOTO/POOL/RAVEENDRAN (Photo credit should read RAVEENDRAN/AFP/GettyImages)
Waziri mkuu wa India Manmohan SinghPicha: AFP/Getty Images

India  imetikiswa  na  maandamano  makubwa  tangu  msichana huyo  mwenye umri  wa  miaka 23 kushambuliwa  kinyama  katika basi  mjini  New Delhi  na  kundi  la  watu  sita.

Serikali  imekuwa  ikijaribu  kulituliza  wimbi  la  hasira  kwa  kuahidi adhabu  kali kwa  uhalifu   mkubwa  unaohusiana  na  ngono  pamoja na  kuunda  tume  maalum  ya  uchunguzi  kuhusiana  na  jinsi  ya kushughulikia  kesi  za  ubakaji.

Polisi wautaka  umma  kuomboleza kwa amani

Wakati maafisa  wakijitayarisha  kwa  ghasia  zaidi mitaani, polisi wameonekana  kuongezwa katika  eneo  la  kati  la  mji  mkuu  wa india   kabla  ya  mwili  wa  msichana  huyo  mwenye  umri  wa miaka  23 haujarejeshwa  nchini  humo. Afisa  wa  polisi  wa  mjini New Delhi  amehimiza  watu kuomboleza  kifo  cha  mwanamke  huyo kwa  amani  wakati  maeneo  kadha  ya  mji  huo mkuu  yamefungwa.

Police detain a demonstrator in front of the India Gate during a protest in New Delhi December 23, 2012. The Indian government moved on Sunday to stamp out protests that have swelled in New Delhi since the gang-rape of a young woman, banning gatherings of more than five people, but still thousands poured into the heart of the capital to vent their anger. REUTERS/Adnan Abidi (INDIA - Tags: CRIME LAW CIVIL UNREST TPX IMAGES OF THE DAY)
Polisi wanajiandaa kwa maandamano makubwa zaidi nchini IndiaPicha: Reuters

Singh , ambaye  hapo  kabla  alitoa  wito  wa  utulivu , amesema kuwa  itakuwa , "Heshima  kubwa  kwa  kumbukumbu  yake  iwapo tutaweza  kuelekeza  hisia zetu hizi  na  nguvu  katika  kuchukua hatua  sahihi."

"Kwa  muda  huu tunahitaji  mjadala  wa  maana  na  uchunguzi kuhusiana  na  mabadiliko  ya  lazima  na  haraka  ambayo yanahitajika  katika  mtazamo  wa  jamii.

"Ni  matumaini  yangu  kuwa  tabaka  lote  la  kisiasa  pamoja  na jamii yote  itatenga maslahi  yao  finyu  ya  binafsi  na  ajenda  ili kutusaidia  kufikia  hatima  ambayo  tunaikusudia, na  kuifanya  india kuwa  mahali  bora  na  salama  kwa  wanawake  kuweza  kuishi.

Mwandishi : Sekione  Kitojo  / afpe

Mhariri: Abdu Mtullya