SiasaAsia
Myanmar yaelezea maendeleo yaliyofikiwa kuelekea uchaguzi
19 Desemba 2024Matangazo
Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Thailand Maris Sangiampongsa. Sangiampongsa alitoa taarifa kwa waandishi wa habari kwamba kulikuwa na mjadala wa wazi kuhusu hali ya Myanmar uliofanyika huko Bangkok, na kusema waliohudhuria walibaini kuwa mkutano huo una umuhimu kwa vile mataifa jirani yanaelewa hali ilivyo vizuri zaidi.
Akinukuu taarifa ya mwenziwe wa mambo ya nje wa Myanmar, Maris alisema utawala wa kijeshi wa taifa hilo uko tayari kwa mazungumzo yatakayojumiisha pande zote zenye nia ya kufanikisha amani ya taifa hilo.