Nairobi. Ujumbe wa IMF kuzuru Kenya.
12 Oktoba 2005Ujumbe wa maafisa wa shirika la fedha la kimataifa IMF utafanya ziara nchinitazuru wiki ijayo kuamua iwapo shirika hilo liruhusu mikopo ambayo imecheleweshwa kutokana na hali ya shaka shaka katika utekelezaji wa hatua za kupambana na rushwa nchini humo.
Mwakilishi mkaazi mwandamizi wa IMF nchini Kenya , Jurgen Reitmaier, amesema kuwa ujumbe huo utafanya uamuzi wa mwisho juu ya iwapo Kenya imetimiza masharti yaliyobaki ili kuweza kukwamua fedha zilizokuwa zimezuiwa Dola milioni 75.
Amesema kuwa ujumbe huo utawasilisha taarifa yake kwa uongozi wa IMF pamoja na bodi ya utendaji, na kama taarifa itakuwa nzuri , fedha hizo zitaweza kutolewa mwezi Desemba.