NAIROBI:Viongozi wa ODM wadokeza mfumo wa kumteuwa mgombea wa urais
22 Agosti 2007Matangazo
Viongozi wa kundi la Orange Democratic Movement nchini Kenya bado wanajadiliana kuhusu nani atakae kuwa mgombea wa urais wa chama hicho katika uchaguzi ujao wa Desemba.
Viongozi hao wamedokeza kwamba watafikia uamuzi huo mwezi Septemba katika mkutano wao mkubwa utakao fanyika katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi.
Rais Kibaki huenda akakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwenye chama hicho.