1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO: Urusi inasaidia mipango ya nyuklia ya Korea Kaskazini

4 Desemba 2024

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami, NATO Mark Rutte amesema Urusi imekuwa ikisaidia mipango ya makombora na nyuklia ya Korea Kaskazini, ili badala yake Pyongyang ipeleke wanajeshi kuisaidia kupambana na Ukraine.

https://p.dw.com/p/4nkKD
Donald Trump empfängt NATO-Generalsekretär Mark Rutte (Archiv)
Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte akihudhuria mkutano na waandishi wa habari, katika makao makuu ya ofisi yake huko Brussels, Ubelgiji Oktoba 1, 2024Picha: Yves Herman/REUTERS

Rutte amewaomba wanachama wa NATO kuipatia Ukraine silaha za kutosha ili kubadilisha mkondo wa vita hivyo, wakati wanajeshi wa Urusi wakizidi kujiimarisha kwenye uwanja wa vita. Amesema hali ni ngumu kwa wanajeshi wa Ukraine kwenye uwanja wa vita kutokana na upungufu wa silaha na rasilimali watu, huku wa Urusi wakizidi kusonga mbele. Rutte amesema hayo alipozugumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa NATO mjini Brussels. Ukraine na washirika wake wanasema Korea Kaskazini imepeleka wanajeshi nchini Urusi kuisaidia kupambana na vikosi vya Moscow kwenye jimbo la Kursk.