New Delhi. India kufungua eneo moja la kuvukia.
7 Novemba 2005Serikali ya India inasema kuwa itaweza tu kufungua eneo moja la mpaka wake kuingia Pakistan leo Jumatatu kuwasaidia watu walionusurika na tetemeko la ardhi lililotokea mwezi uliopita katika jimbo la Kashmir.
Pande zote mbili zinamatumaini ya kufungua maeneo matano katika mipaka yao. Maafisa wa India wanasema kuwa eneo lingine litafunguliwa siku ya Jumatano na la tatu litafunguliwa siku ya Alhamis.
Wanasema kuwa kazi ya kusafisha njia kuingia katika jimbo hilo, inayohusisha kuondoa mabomu ya kutegwa ardhini inaendelea. Hatua hiyo inaonekana kuwa ni ishara ya kukaribiana kwa urafiki kuliko hatua ambayo inaweza kuwa na manufaa makubwa kwa wale walionusurika katika jimbo hilo.
Tetemeko la ardhi la mwezi uliopita limeuwa zaidi ya watu 73,000 katika eneo la jimbo linalodhibitiwa na Pakistan la Kashmir na jimbo la kaskazini magharibi, wakati watu 1 300 wamekufa katika eneo linalodhibitiwa na India la Kashmir.