1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI : India na Pakistan zafikia makubaliano muhimu

7 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEnE

Nchi jirani zenye silaha za nuklea India na Pakistan zimekubali kutaarifiana rasmi juu ya majaribio ya makombora ya nuklea ya nchi zao na hiyo kuimarisha mchakato wa amani kati ya nchi hizo.

Mazungumzo ya karibuni kabisa yaliofanyika New Delhi nchini India yalikuwa ni sehemu ya jaribio la kutatuwa mzozo wao uliodumu kwa miongo kadhaa juu ya jimbo la Kashmir.Nchi hizo mbili pia zimekubaliana kuanzisha mawasiliano ya haraka ya moja kwa moja kati ya maafisa wao waandamizi katika wizara za mambo ya nje.

Mahasimu hao wawili wa Asia ya Kusini waliishtusha dunia kwa kufanya majaribio ya nuklea hapo mwaka 1998.