NEW DELHI: India na Pakistan zakubali kuimarisha uhusiano
17 Aprili 2005Matangazo
Rais Pervez Musharraf wa Pakistan na waziri mkuu Manmohan Singh wa India wamekutana mjini New Delhi.Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya India,mkutano huo uliofanywa katika mazingira ya kirafiki,unaridhisha.Vyomba vya habari nchini India vimesema viongozi hao wawili wamekubaliana kuchukua hatua za kupunguza mivutano na kuboresha uhusiano wa kibiashara na misafara ili kuimarisha mwenendo wa amani kati ya madola hayo mawili yenye nguvu za kinuklia.Lakini hakuna ishara kuwa kumepatikana maendeleo fulani kuhusu suala la Kashmir.Tangu Pakistan na India kujipatia uhuru kutoka Uingereza mwaka 1947,nchi hizo zimepigana vita mara mbili kwa sababu ya jimbo la Kashmir.