NEW DELHI : India na Pakistan zazungumzia amani
14 Novemba 2006Matangazo
India na Pakistan zimeanza tena mazungumzo yao ya amani baada ya pengo la miezi minne kufuatia mashambulizi ya kigaidi mjini Mumbai hapo mwezi wa Julai.
Maafisa wa serikali ya India wanaamini kundi linaloungwa mkono na Pakistan lilikuwa limehusika na mashambulizi hayo yaliopelekea kuuwawa kwa watu 186 na kujeruhi wengine 800.
Mazungumzo hayo katika mji mkuu wa India New Delhi yanatazamiwa kulenga jimbo lenye mzozo la Kashmir na hatua za pamoja za kupiga vita ugaidi.