1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New-Delhi: India na pakistan,mahasimu wawili wenye kumiliki silaha za...

26 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFy0
kinuklea,wamekubaliana kuweka chini silaha katika mzozo wa miaka 14 wa kuania jimbo la Kashmir.Makubaliano ya kuweka chini silaha yameanza kufanya kazi usiku wa manane wa kuamkia leo.Unalihusu eneo zima linaloigawa Kashimir sehemu mbili katika milima ya Himalaya.Muda mfupi kabla ya hapo watoto watatu waliouliwa kwa risasi za wanajeshi wa India.Madola yote mawili,India na Pakistan yameweka malaki ya wanajeshi walioshamiri silaha katika eneo hilo.Yameshateremka mara mbili vitani kuuania jimbo la Kashimir.Makubaliano ya kuweka chini silaha hayawahusu wanamgambo wa kiislam wanaokutikana katika sehemu ya India ya jimbo hilo.Wanadai uhuru kamili au kuunganishwa neoe lao na Pakistan.India imekua ikiilaumu Pakistan kuwaunga mkono waasi.