NEW DELHI: India yajaribu kombora linaloweza kubeba mabomu ya kinuklia
19 Novemba 2006Matangazo
India imefanikiwa kujaribu kombora la masafa ya wastani ambalo huweza kupachikwa mabomu ya kinuklia.Kwa mujibu wa afisa katika wizara ya ulinzi,kombora la Prithvi II lilirushwa kutoka jimbo la pwani ya mashariki la Orissa.Jaribio hilo limefanywa siku tatu baada ya Pakistan kufanya jaribio la kombora lake la Ghauri linaloweza kubeba mabomu ya kinuklia.India iliarifiwa na Pakistan kuhusu jaribio hilo na wakati huo Pakistan ikasema kuwa inaitazamia India kufanya jaribio lake hivi karibuni.