1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI : India yawasaka wahusika wa miripuko ya mabomu

30 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CENP

India imekuwa katika msako wa kuwatafuta watu waliohusika na miripuko ya mabomu iliyouwa watu 60 mjini New Delhi watuhumiwa wakuu wakiwa ni wanamgambo wanaopinga mchakato wa amani na Pakistan.

Miripuko hiyo imetokea kwenye basi na katika masoko mawili yaliokuwa yamejaa watu hapo jana usiku wakati wanadiplomasia wa India na Pakistan wakiwa ndio kwanza wakikamilisha makubaliano ya kufunguwa mpaka wao katika jimbo linalogombaniwa la Kashmir kwa ajili ya shughuli za misaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi.

Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh ameapa kwamba India haitosalimu amri kwa ugaidi wakati Pakistan kwa haraka imelaani mashambulizi hayo ambayo inaonekana yamekusudia kusababisha maafa makubwa wakati wananchi wakijiandaa kwa manunuzi kwa ajili ya sherehe za Diwali.

Sing amewaambia waandishi wa habari leo hii kwamba magaidi wanataka kueneza hisia ya hofu na tuhuma miongoni mwa wapenda amani.