New Delhi: Maafa ya vifo na mafuriko kutokana na Mvuwa za Masika huko Orissa,India.
3 Septemba 2006Matangazo
Mafuriko yaliosababishwa na mvuwa za masika mnamo siku chache zilizopita yameawaacha watu milioni 1.5 wakiwa hawana majumba na kuharibu maelfu ya ekari za mashamba katika Mkoa wa Orissa, nchini India. Maafisa walisema jana kwamba zaidi ya watu 20,00 wameokolewa baada ya mamia ya vijiji kukatwa. Wanajeshi walikuwa wakiwaokoa wanavijiji zaidi kutoka wilaya za mwambao, huku kukitarajiwa mvuwa zaidi. Katika Mkoa wa Orissa mvuwa zisizokwisha na mafuriko katika miezi mitatu iliopita zimeshawauwa watu 70 na kuharibu barabara na umeme.