NEW DELHI-Mabasi mawili yashambuliwa na wanamgambo katika eneo la Ksahmir linalomilikiwa na India.
7 Aprili 2005Mabasi mawili yaliyokuwa yakitokea eneo la Ksahmir linalomilikiwa na India,yakielekea upande wa Kashmir wa Pakistan yameshambuliwa kwa risasi na waasi.
Msemaji wa polisi mjini Salamabad upande wa India,amesema hakuna aliyejeruhiwa katika shambulio hilo.Msemaji huyo amesema risasi hizo zilivurumishwa kutokea eneo la karibu na mabasi hayo,yaliyokuwa yakisafiri kutokea Srinigar,mji unaomilikiwa na Indoa wa Kashmir kwenda Muzaffarabad upande wa Pakistan.
Hii ni huduma ya kwanza ya usafiri wa mabasi kuunganisha pande mbili za mkoa wa Himalaya kwa kipindi cha karibu miaka 60.Mabasi hayo yalikuwa yamewachukua zaidi ya abiria 20 na yalikuwa yakisindikizwa na msafara wa wanajeshi.
Wanamgambo wanaopigana kuondoa utawala wa India katika Kashmir,walitishia kushambulia msafara huo wa mabasi.